Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 16.08.2018:


Kiungo wa kati mshambuliaji wa Manchester City Kevin de Bruyne kutoka Ubelgiji mwenye miaka 27 anatarajiwa kutocheza kwa miezi mitatu baada ya kuumia kwenye kano za goti la kulia. (Mirror)

Baadhi wanatarajiwa De Bruyne hataweza kucheza kwa miezi miwili hadi minne kutokana na jeraha hilo lake la goti. (Telegraph)

Kevin De Bruyne aumia akifanya mazoezi
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alimwambia Paul Pogba anafaa kuwasilisha ombi la kutaka kuondoka iwapo hataki kusalia katika klabu hiyo. Mfaransa huyo mwenye miaka 25 naye amemjibu Mreno huyo kwa kumwambia kwamba atawasiliana naye kupitia kwa wakala wake pekee. (Sun)

Bayern Munich wanamnyatia beki wa Tottenham mwenye miaka 29 anayetokea Ubelgiji Toby Alderweireld. (Mirror)

Kipa wa Arsenal mwenye miaka 29 kutoka Colombia David Ospina amejiunga na Napoli kwa mkopo. (Guardian)

Parma wanakaribia kumnunua mshambuliaji wa Ivory Coast mwenye miaka 31 Gervinho kutoka klabu ya Hebei Fortune ya China wanapojiandaa kurejea kucheza katika Serie A. (Mediaset - in Italian)

Liverpool wamekataa ofa kutoka kwa Torino ambao wamekuwa wakimtaka kiungo wa kati wa Serbia mwenye miaka 22 Marko Grujic. Klabu hiyo ya Italia ilikuwa inamtaka mchezaji huyo kwa mkopo wa msimu mmoja na uwezekano wa kumnunua kikamilifu kwa bei ya £9m mwaka ujao. (Liverpool Echo)

Klabu ya Sydney FC ya Australia inafanya mazungumzo na mshambuliaji wa England mwenye miaka 31 Adam Le Fondre. Mchezaji huyo hana mkataba wowote baada yake kuondoka Bolton Jumanne. (Fox)

De Bruyne huenda asiweze kucheza tena kwa miezi mitatu
Kiungo wa kati wa Newcastle kutoka Senegal mwenye miaka 27 Henri Saivet anakaribia kujiunga na klabu ya Bursaspor ya Uturuki kwa mkopo. (Evening Chronicle)

Winga Mfaransa mwenye miaka 23 anayechezea Tottenham Georges-Kevin N'Koudou anatarajia kuhamia klabu ya Mainz ya Ujerumani kwa mkopo. (Sky Sports)

Atletico wawashinda Real Madrid bila Ronaldo
Bao la Ronaldo kushindania tuzo ya bao bora la msimu Ulaya
Sergio Ramos amshutumu meneja wa Liverpool
Blackburn Rovers wamewasilisha ofa ya £6m kumtaka kinda mshambuliaji wa England wa miaka 19 anayechezea Nottingham Forest Ben Brereton. (Sun)

Meneja wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinezanataka sana kumchezesha mchezaji wa Manchester United Andreas Pereira lakini kiungo huyo wa kati mwenye miaka 22 anadaiwa kutaka kuichezea Brazil, nchi walimotoka wazazi wake. (UOL)

Chelsea wanamtafuta mtu wa kujaza nafasi ya mkurugenzi wa uchezaji Michael Emenalo, na inaarifiwa wakurugenzi wa kiufundi wa Chama cha Soka cha England (FA) Dan Ashworth, Juliano Belletti, Michael Ballack, na mkurugenzi wa uchezaji wa Roma Monchi ni miongoni mwa wanaoangaziwa. (Telegraph)

Klabu moja ya Uturuki inayoibukia iliwauza wachezaji wake 18 chipukizi ili kutafuta pesa za kugharimia ununuzi wa mbuzi 10. Mpango wao ni kutumia maziwa ya mbuzi hao na nyama kufadhili shughuli zake za kifedha siku za usoni. Maajabu hayo, mbuzi na wachezaji nani ana thamani kubwa? (Hurriyet)


Mkufunzi wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane anataka kurudi katika kazi yake ya ukufunzi na anajiandaa kumrithi Jose Mourinho katika klabu ya Manchester United msimu ujao. (L'Equipe)

Mkurugenzi wa Barcelona Ariedo Braida anasema klabu yake haiwezi kutoa ofa kwa Paul Pogba wa Manchester United msimu huu, lakini amemtaja mchezaji huyo Mfaransa mwenye miaka 25 kama mchezaji mzuri na atakuwa anamfuatilia Mfaransa huyo. (Mirror)

Klabu ya Bundesliga ya Schalke wana mpango wa kutoa mikataba ya kudumu na hawana nia ya kuwasaini beki wa Tottenham raia wa England Danny Rose, 28, au kiungo wa kati wa England Ruben Loftus-Cheek, 22, kwa mkopo. (Sky Sports)

Meneja mpya wa Chelsea Maurizio Sarri amelegeza sheria kali kuhusu lishe na ratiba za mechi zilizowekwa na mtangulizi wake Antonio Conte. (Telegraph)

Sarri yuko radhi kiungo wa kati wa Chelsea mwenye miaka 28 Danny Drinkwater auzwe mwezi huu. (Star)

Lionel Messi
Lionel Messi hatacheza kwenye mechi yoyote ya Argentina na haijulikani iwapo mshambuliaji huyo wa Barcelona mwenye miaka 31 atacheza tena mechi za kimataifa. (Clarin)

Meneja wa Arsenal Unai Emery atalazimika kubana matumizi kwenye klabu msimu ujao kwa kununua wachezaji. (Telegraph)

Uwanja mpya wa Tottenham hatakuwa tayari ifikapo Novemba na klabu hiyo itakuwa ikichezea mechi zake zote za nyumbani huko Wembley. (Times)

Mlinzi wa Atletico Madrid raia wa Uruguay Diego Godin, 32, alikataa ofa ya kuhamia Manchester United kutokana na sababu za kibinfasi. (Mirror)

Source BBC.

Nifate Instagram kwa jina la @pasien9

Comments

Popular posts from this blog

COMBAT THEFT; How can I track a phone through its IMEI number?

6 Home Businesses You Can Start With No Money

FAHAMU KUHUSU VIRUSI VYA CORONA.