Kipa yupi ni bora kuwahi kutokea Manchester United kati ya hawa?
Source : shaffihdauda.co.tz
Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu ni nani kipa bora aliyewahi kuichezea Manchester United kati ya Schmeichel, Van Der Saar na David De Gea, wakati huu ambapo kuna taarifa ya De Gea kudaka dili jipya United ni vyema tuwatazame wote watatu kwa mataji yao na wewe uamue yupi alifanikiwa zaidi.
Peter Schmeichel.
Wakati Schmeichel akijiunga na Manchester United kulikuwa na uhaba mkubwa wa makombe, na 1991 alipojiunga na United akitokea Brondby, msimu uliofuata walichukua kikombe cha EPL.
Makombe ya Schmeichel.
EPL (1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99) FA Cup (1993-94, 1995-96, 1998-99) League Cup (1991-92) FA ngao ya Hisani (1993, 1994, 1996, 1997) Champions League (1998-99) UEFA Super Cup (1991).
Tuzo binafsi.
Kipa bora wa Dernmark (1987, 1988, 1990, 1992) Kipa bora wa UEFA(1992, 1993, 1998) IFFHS World’s Best Goalkeeper (1992, 1993) Kipa bora wa UEFA vilabu (1997-98).
Edwin Van Der Saar.
Mwaka 2005 Manchester United walimsaini Van Der Saar kwa ada ndogo tu £2m kutoka Fulham, United wakiamini kwamba huyu alikuwa mrithi haswa wa Petre Schmeichel, akiwa United alibeba jumla ya makombe 11 huku mwaka 2009 akiweka rekodi kucheza dakika nyingi bila kufungwa(dakika 1311).
Makombe ya Van Der Sar.
Premier League (2006-2007, 2007-2008, 2008-2009, 2010-2011) League Cup (2005–2006), FA Ngao ya Hisani (2007, 2008, 2010) Champions League (2007-2008) FIFA Club World Cup (2008).
Tuzo binafsi.
Kikosi cha Epl (2006-2007, 2008-2009, 2010-2011), Kikosi cha UEFA (2008) Premier League Merit Award (2008-2009), kipa bora wa UEFA (2009).
David De Gea.
United walimnunua kutoka Atletico Madrid mwaka 2011 kwa ada ya £19m na kuamini huyu ndio mrithi wa Van Der Saar, amekuwa mhimili haswa kwani tangu SAF aondoke United De Gea amekuwa mchezaji pekee ambaye kiwango chake hakijawahi kushuka huku hadi saaa akicheza michezo 238 kwa United.
Kuna vitu vingi United wanaamini De Gea ni bora, tofauti na makipa ambao walitangulia walikuwa wakilindwa na wakina Vidic, Evra, Roy Keane na walinzi wengine nguli wa zamani United, De Gea ni kipa mwenye ulinzi dhaifu na matokeo chanya.
Makombe ya David De Gea.
Epl (2012-2013), FA Cup (2015-2016), kikombe cha ligi (2016-2017) Europa League (2016-2017), Ngao ya hisani (2011, 2013, 2016),
Tuzo binafsi.
Mchezaji wa mwaka wa PFA (2014), tuzo ya Sir Matt Busby (2013-2014, 2014-2015, 2015-16, 2017-2018), tuzo ya mchezaji bora Manchester United (2013-2014, 2014-2015, 2017-2018)
ENDELEA KUWA NAMI KWA HABARI MOTOMOTO.
Comments
Post a Comment