Haji Manara awatolea povu zito Wanasimba.
Haji Manara awatolea povu zito Wanasimba, “Uturuki hatukwenda jifunza mpira, tulieni”
Baada ya ushindi mwembamba wa simba dhidi ya Prisons Haji Manara awatolea povu zito Wanasimba, na kusema kwamba “Uturuki hatukwenda jifunza mpira, tulieni”.
Mpira bwana una raha zake na mashabiki wa soka wanaufanya mpira uwe kati ya mchezo mtamu sana ulimwenguni, malalamiko pamoja na vioja vyao ndio raha ya soka.
Mnyama leo alikuwa uwanjani kukipiga dhidi ya timu ya Tanzania Prisons ya jijini Mbeya na bao pekee la Meddy Kagere liliwafanya Simba kuibuka na alama zao tatu muhimu.
Tangu mchezo ukiendelea kulikuwa na minong’ono ya mashabikiwa Simba uwanjani kuhusu mfumo wa kocha wao Patrick Asseums wakidai hafai na timu yao haikupaswa kupata ushindi mwembamba hivyo.
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara naye ameyasikia maneno ya mashabiki wa Simba na Manara kama kawaida yake ameshindwa kukalia kimya suala hilo na kuamua kuwajibu.
“Wakati mwingine najiuliza wanadamu haswa mashabiki wa mpira wanataka nini, nimetalii kidogo kwenye magroup machache ya Wanasimba whtaspp nimeshangazwa kuona kutoridhishwa kwao na matokeo ya leo
Wengine kwenye Instagram wamefikia mbali zaidi na kusema hawaridhishwi na mfumo wa kocha wetu, guys mpira ni Sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kufanya upasuaji
Ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba haujui mpinzani wako kajipangaje wala hujui wachezaji wako wakoje, lakini ukubwa wa Sayansi hii hauna jibu la moja kwa moja kama ilivyo hesabu kwamba 3 mara 3 ni tisa.
Mara nyingi nakataa kuwa katika group za whatsapp kwa sababu mpira wameujulia mtandaoni hawana shibe ya mchezo huu adhimu kabisa kwao hudhani kila siku lazima Simba itashinda na lazima ipate bao saba au tano.
Wanasahau kwamba Prisons iliingia Top Four mwaka jana, na wanasahau Prisons haifungiki kirahisi kama Mnyela United halafu wanakuja na hoja iliyopaliliwa na wanazi wa nazi chai eti team imetoka Uturuki why ishinde moja?
Afanaleki hapo Haji naonekana mtata, aliowaambia tulienda Uturuki kujifunza mpira ni nani? Kule tulikwenda camp ya pre season, ni mazoezi ya mwanzo wa msimu na wengine walienda Zanzibar kama ilivyo Prisons na wapo walioenda hadi Mkamba kote huko ilikuwa inatafutwa Chemistry ya mpira.
Ni vyema mkijifunza mchezo huu mjifunze na Sayansi yake, na sio munajifunza kirahisi rahisi tu kama Sayansi Kimu , leo tulicheza na timu nzuri na wamejiandaa kama tulivyojiandaa sisi.
Ni lazima muelewe mfumo wa kocha hauji kwa kipindi kifupi, unachukua muda kidogo. Niwasihi Wanasimba soka ni mchezo wa draft au chess na sio Kisaprov Kisaprov, inabidi shabiki kabla ya kulaumu ujue vitu vingi kwenye medula yako, vinginevyo ni kufanya uchale tu.
Comments
Post a Comment