UPDATES KESI YA NONDO
Kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo amekutwa na kesi ya kujibu kwa mashtaka mawili yanayomkabili mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Iringa.
Nondo, ambaye alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza mwezi Machi mwaka huu anakabiliwa na mashtaka ya kutoa taarifa ya uongo kwa ofisa wa polisi wa kituo Mafinga akidai alitekwa na watu wasiojulikana.
Katika shtaka la pili, Nondo anadaiwa kutoa taarifa za uongo mtandaoni.
Hakimu Liad Chamchama katika maamuzi yake leo Agosti 27 amesema kuwa baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyotolewa na upande wa Jamhuri korti imejiridhisha kuwa mtuhumiwa ana kesi ya kujibu.
Mahakama imepanga Septemba 18 na 19, 2018 kuanza kusikiliza mashahidi wa upande wa utetezi.
Wakili wa Nondo, Jebra Kambole ameiambia BBC kuwa hawajastushwa na uamuzi wa mahakama na wamejipanga kwa utetezi madhubuti.
"Tumejitayarisha. Tuna mashahidi watano na Nondo mwenyewe atajitetea ili watu wote wajue hasa nini kilimtokea," amesema wakili Kambole.
Toka alipopandishwa kizimbani mwezi Machi mwaka huu, Abdul Nondo ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesimamishwa masomo na uoungozi wa chuo hicho mpaka pale kesi hiyo itakapofikia tamati.
AAAAAAAAAAAAAA
ReplyDelete