FAHAMU KUHUSU VIRUSI VYA CORONA.
Tabia za pamoja
Virusi vya corona huwa na uwezo wa kubadilika na aina nyingi husababisha magonjwa yasiyo hatari sana upande wa binadamu. Kudhoofika kwa mwili kutokana na mashambulio ya virusi kunafungua milango kwa bakteria wabaya kukuvamia na kusababisha maambukizo ya mfumo wa upumuo, kama mafua au homa ya mafua (influenza), yanayoishia kwa kawaida baada ya siku kadhaa, lakini kuna pia maambukizo ya hatari kama nimonia inayoweza kusababisha kifo. Hivyo inatakiwa watu wapunguze kutumia kwa pamoja vitu hatarishi kama vile vya ncha kali[4].
Hadi sasa hakuna chanjo au dawa ya kudhibiti virusi vya aina hii. Kwa hiyo uponyaji hutegemea mara kwa mara nguvu ya kinga mwilini cha kila mtu. Hii inamaanisha virusi hivi huleta hatari hasa kwa watu wenye kinga cha mwili kilichodhoofishwa.
Aina hizo za virusi zina uwezo wa kubadilika, miaka ya nyuma ulikuwa na mabadiliko kadhaa yaliyosababisha vifo vya watu na kuenea haraka kimataifa, hivyo kusababisha hofu za epidemiki au hata pandemia.
CHANZO: TOVUTI YA WIKIPEDIA
Comments
Post a Comment