KWANINI JANUARI NDIYO MWANZO WA MWAKA?
Jinsi ilivyoamuliwa kwamba Januari ndio mwezi wa kwanza wa mwaka Kila mwaka tarahe kama hii watu kutoka kote duniani hukaribisha mwaka mpya kwa fataki, kupiga filimbi, pambaja na vinywaji. Lakini kabla ya kuanza sherehe hizo je hujafikiria ni kwa nini tarehe mosi Januari ndio inayoadhimisha kuanza kwa mwaka mpya? Kila kitu kinatokana na mila na tamasha za Roma, na kalenda iliozinduliwa na Julius Caesar miaka 2000 iliopita. Lakini pia huwezi kumwacha nje papa aliyejulikana kwa jina Gregorio wa kumi na tatu. Hebu tuone ni kwa nini? Kwa Waroma wa zamani .Januari ilikuwa muhimu kwa sababu ulikuwa mwezi uliotakaswa kwa mungu Janus (hivyobasi ukaitwa Ianuarius, ikimaanisha Januari kwa kilatino.} "Inahusishwa na kuangalia mbele na nyuma," anaelezea Diana Spencer, profesa katika Chuo Kikuu cha Birmingham nchini Uingereza. "Kwa hiyo ikiwa kuna muda katika mwaka ambao unapaswa kuamua, huu ndiyo wakati tunapoanza tena." Ni mantiki kuwa...